Jumanne, 11 Juni 20130 comments




UFUGAJI WA NG'OMBE



Ng'ombe wa kienyeji ndiyo wanaofugwa kwa wingi Tanzania bara na Visiwani ikiwa ni asilimia 96.2 bara na asilimia 95.2 visiwani. Ng'ombe wa nyama na maziwa walioboreshwa ni asilimia (0.9 na 2.9) kwa bara na asilimia (0.7 na 4.1) kwa visiwani. Idadi ya ng'ombe Tanzania bara na visiwani inaonekana kupongezeka ukilinganisha na ya sensa ya mwaka 2002/2003 kwa ng'ombe 4,281,082. Takwimu hizi zinaonyesha kuwa mkoa wa Shinyanga ndio unaofuga ng'ombe wengi zaidi ikifuatiwa na Tabora. Mikoa mingine inayofuga ng'ombe wengi kuanzia milioni moja hadi mbili ni Mwanza, Arusha, Mara, Manyara, Singida and Dodoma 

Chanzo: (Repoti ya taifa iliyotolewa mwezi wa tatu mwaka huu inayotokana na sensa iliyofanyika mwaka 2007/2008 kwa kutumia sampuli).
Share this article :

Chapisha Maoni

 
Copyright © 2013. KCC KIBAHA - All Rights Reserved
Template Created by KIJANA WA LEO Published by TITUS KAPOMA
Proudly powered by Blogger