Jumanne, 11 Juni 20130 comments


UFUGAJI WA KUKU
ATHUMANI IDDY KIMISHA
UTANGULIZI
Kuku yupo katika kundi la ndege wanaofugwa na binadmu, katika kundi hili la ndege
wa kufugwa wapo pia bata, bata mzinga, bata bukini,
njiwa, na kanga. Njiwa, bata na
bata mzinga walianza kufugwa zaidi ya miaka 3,000 iliyopita nchini China. Kuku nao
yasemekana walianza kufugwa miaka hiyohiyo wakitolewa katika misitu ya ndege ya
Kiasia. Baaday ndege wakaanza kufugwa sehemu mabalimbali za bara la Marekani
na Ulaya wakiwa
fuga kwa njia ya kienyeji. Mnamo karne ya 16 kuku waliingia
Marekani wakitokea Ulaya na bata mzinga wakaingia Ulaya wakitokea Marekani.
Njia za kisasa za uanguaji wa mayai zilianza kutumika miaka ya 1870 lakini si kwa
hatua ya kibiashara katika nchi za Chi
na na Misiri ya zama hizo. Ufugaji wa ndege
kwa njia ya kisasa ulianza kutumika kuanzia karne ya 19 katika bara la Marekani na
Ulaya wakilenga katika uboreshaji wa nyama na mayai. Tafiti na mbinu mbalimbali
za ujengaji wa nyumba, ulishaji wa ndege, na uzal
ishaji wa kuku zilizoibuliwa
zilipelekea kukua kwa kasi kwa ufugaji wa ndege na hasa kuanzia miaka ya 1930.
Laikini ufugaji huu na ulaji wa ndege na mazao yake uliongezeka kwa kiasi kikubwa
zaidi wakati wa vita kuu ya pili ya dunia kulipotokea uhaba wa nya
ma ya ng'ombe na
nguruwe.
Nchini Tanzania haijulikani ni lini ufugaji wa ndege ulianza kufanyika, lakini huenda
ulianza mara baada ya kuanza kuwa na makazi kutohamahama na hasa wakati wa
utawala wa mkoloni. Kulingana na sensa ya mwaka 1994, idadi ya ndege
iliyokuwa
inafugwa wakati huo ilikuwa ni
29 685 220 na kati ya hawa kuku wa kienyeji
walikuwa
20 163 811 na wa kisasa walikuwa 521 411 (wa nyama
-
368, 933 na wa
mayai
-
152 478). Ndege wengine wakiwa bata na bata bukini
743 472, bata
mzinga
63 447, na kanga
37 942. Idadi hii imeongezeka sana kwa miaka ya karibuni
kulingana na watu wengi kuvutiwa na ufugaji wa kuku na ndege wengine kwasababu
ya faida zinazopatikana kwenye ufugaji wa ndege. Makadiro ya mwaka 2008
yalionyesha kuwa Tanzania ilikuwa na kuku milion
i 36 na kati ya hao asilimia 95 ni
kuku wa kienyeji, waliobaki ni wa kisasa.
FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU
Ukimtaja kuku katika maisha ya Mtanzania hakuna asiyemfahamu ama kwa
kumuona au kwa kumla na hivyo kufanya kuwa kitu muhimu sana katika maisha ya
kila si
ku. Asilimia kubwa ya Watanzania wanafuga kuku tena kuku wa kienyeji au
kwa jina jingine kuku wa kijijini kwa vile asilimia kubwa (80%) ya wafugaji wa kuku
wa kienyeji wapo vijijini. Kwa udogo wake, kuku amekuwa ndo mnyama rahisi wa
kuchinja kwa kitoweo ny
umbani, wajapo ndugu, jamaa na marafiki kutembelea
familia. Hivyo kuku hawa wanafugwa kwa malengo makuu mawili; kwa ajili ya
matumizi madogo madogo ya nyumbani na kwa ajili ya kuongeza kipato katika
familia. Kuku anafaida zifuatazo;
1. Kutumika kwa chakul
a na hivyo kupunguza tatizo la upatikanji wa protini katika
familia
2. Kusaidia kuongeza kipato katika jamii na kusaidia kutatua matatizo kwa haraka
zaidi maana uuzaji wake ni rahisi.
3. Kuku (jogoo) wamekuwa wakitumika tangu enzi kama saa ya familia wakat
i
wanapotaka kuamka usiku kwa shughuli mbalimbali
Kuku ni mkombozi wa watu wenye kipato cha chini na watu wengi wanapenda
kufuga kuku kwa sababu zifuatazo;
1. Watu wengi hasa mijini wanapenda kula nyama ya kuku na mayai hasa kuku wa
kienyeji
2. Uwekezaji w
a ufugaji wa kuku ni mdogo na hivyo kufanya watu wengei waweze
kufuga kuku
3. Upatikanaji wa chakula cha kuku ni rahisi
4. Kuku wanahitaji muda mfupi sana kukua na hivyo faida yake inaonekana mapema
5. Urahisi wa upatikanaji wa dawa na chanjo
5. Gharama za matunzo ni ndogo na hasa kuku wa kienyeji
KUANZA KUFUGA KUKU
Ufugaji wa kuku chinin Tanzania upo wa aina kuu mbili, ufugaji wa kuku wa kienyeji
na ufugaji wa kuku wa kisasa. Na kama tulivyokwisha kuona hapo juu ufugaji wa
kuku wa kienyeji nd
iyo wenye watu wengi zaidi na hii ni kutokana na ufugaji huo
kuwa rahisi na usio na gharama kubwa.
Kabla ya kuanza ufugaji wa kuku (aina yeyote ile) kuna mambo ya msingi ya
kuzingatia ili ufugaji wako uwe endelevu na wenye kukuletea manufaa makubwa na
faa
ida zilizoainishwa hapo juu. Mtu yeyote anayetaka kufuga kuku lazima awe na
dhamira ya dhati ya kutaka kufuga kuku maana kwa njia hii atawafuatilia kwa ukaribu
na kuwapa mahitaji ya msingi ili waweze kuzaa matunda yaliyotarajiwa. Anapaswa
akae chini na kup
anga kabla ya kuanza ufugaji wake, sehemu hii ya awali ya
muhimu na haipaswi kurukwa na tena anayetaka kufuga kuku
ni vema akapata
ushauri toka kwa wataalamu wa mifugo au wafugaji wengine wenye uzoefu.
Anatakiwa ajue ni aina gani ya ufugaji anataka kufany
a (wa kuku wa kienyeji au wa
kisasa), kuku wa nyama au wa mayai. Yote haya yatategemea na mahitaji ya eneo
alipo pamoja na mambo manne ya msingi ya mtaji, shamba/eneo la kufugia,
usimamizi na masoko.
KUKU WA KIENYEJI
Ufugaji wa kuku wa kienyeji hasa kwa n
chi yetu ndiyo unaongoza kwa kuwa na
wafugaji wengi na wengi wapo kijini. Sababu kubwa ni kwamba ndio ufugaji rahisi na
unaohitaji mtaji mdogo kuanzisha na kuku huvumilia sana magonjwa na adha
nyingine za kimazingira. Ufugaji wa kuku wa kienyeji unasaidia
kukidhi mahitaji ya
kiuchumi na kibiashara kwa familia masikini za vijini. Mbali na kwamaba kuku hawa
wa kienyeji hutumiwa kama kitoweo mara kwa mara katika jamii, lakini pia kuku
hawa huuzwa kuongeza kipato kinachosaidia familia kununua chakula madawa,
ng
uo, kulipia kalo za shule kwa wanafunzi, pembejeo za kilimo, kutoa mahali,
kwenye matibanu ya asili pamoja na mambo mengine ya kimila. Ufugaji wa kuku
vijijini umeonekana kuwa njia mbadala ya kuongeza kipato na kusaidia kutatua
matatizo ya wanancho hasa wa
kati ambapo mazao yao hayako tayari kwa kuyauza
kutokana na kutokomaa au bei kuwa chini.
Kwa vile asilimia kubwa ya wafugaji wa
kuku wa kienyeji wapo kijijini nitajikita zaidi
kuelezea ufugaji wa vijijini kwa vile ule wa mijini unakaribiana sana na ule wa
kisasa.
Kuna aina mbalimbali za kuku wa kienyeji wanaofugwa Tanzania na wafugaji wa
wadogo. aina hizi zinatofautiana kwa umbo,
uwezo wa kutaga na kuangua mayai,
idai ya mayai wanayotaga na utunzaji wa watoto. Majina na aina ya kuku
wanatofautina kulingana na eneo walikoanza kufugwa. Kuku wa kienyeji hutaga kwa
wastani mayai 8
-
15 na aslimia 80 ya mayai yaliyoatamiwa huanguliwa. Ku
ku wa
kienyeji hutaga mara 2
-
3 kwa kila mwaka.
Wafuatao ni baadhi ya aina ya kuku wa
kienyeji waliokwisha tambuliwa na sifa zao:
Kuchi au Kuza
-
Hawa wana midomo mifupi na manyoya machache, wazitona
wenye nyama nzuri, hutaga mayai machache 7
-
10 lakini huyaa
ngua
yote, utagaji
wao ni kila baada ya miezi 4, wanapendwa sana na watu kwasababu ya ukubwa na
uzito wao.
Poni au Kishingo
-
Umbo dogo, uzito mdogo, manyoya mengi, hutaga mayai hadi 20
na kuyaangua yote,
utagaji wao ni kila baada ya miezi 4, ni walezi wazu
ri wa
watoto.
Mbuni
-
Wana ukubwa wa kati, hawana mkia, hutaga mayai hadi 15 na huyaangua
yote,
utagaji wao ni kila baada ya miezi 3
-
4,
hupata magonjwa kirahisi.
Tongwe au msumbiji
-
Hawa ni wafupi, thabiti, wenye umbo dogo na uzito
mdogo,
hutaga mayai hadi
20 na kuyaangua yote,
utagaji wao ni kila baada ya miezi
3
-
4, walezi wazuri wa watoto, wanapendwa sana na wafugaji lakini si wanunuzi
kwasababu ya umbo dogo.
1.Mtaji
Ufugaji wa kijijini unafanywa kwa kuwaacha kuku watafute chakula wenyewe
wakitembea huku
na kule kuokoteza chakula au mizoga. Hii inafanya gharama ya
ufugaji kuwa ndogo, mtaji mdogo na ufugaji wenyewe kusimamiwa na mama na
watoto.
a)
Nyumba ya kuku
Mara nyingi kuku hawa huko vijijini wanalala nje au ndani ya nyumba wanamolala
binadamu. Wengine wamekuwa wakiwalaza kuku kwenye kona ya nyumba
wanamolala, wengine kuwatengea chumba kimojawapo ndani ya nyumba
wanamolala na baadhi kuwalaza kuku kwenye vihen
ge vya kienyeji au kwenye
mabanda ya kuota mota na jikoni wanako pikia vyakula na wengine wachache
huwalaza juu ya miti. Ni asilimia ndogo sana wanaodiriki kuwajengea mabanda kuku
wao, tena hasa kwa wakati huu ambapo hamasa ya ufugaji imongezeka kwa
kutamb
ua thamani ya kuku wa kienyeji. Vifaa kwa ajili ya ujenzi vinapatikana kwa
urahisi katika eneo husika, kama tofali, miti, udongo na majani ya kuuzekea nyumba
au mabanda ya kuku. Katika mazingira ya ufugaji wa kijiji mara nyingi kuku wengi
hulazimika kulala
kwa kubanana na hewa pia huwa si ya kutosha kwa kuku.
Mijini nako wameona thamani ya ufugaji wa kuku na hasa wa kienyeji ni kutokana na
kuongezeka kwa soko la kuku wa kienyeji kwa vile nyama yake haina kemikali
nyingi. Hawa wanafuga kwa kuwajengea kuku m
abanda yao nje ya nyumba wanamo
lala.
b)
Chakula na Lishe
Kuku wa kienyeji mara nyingi hujitafutia chakula wenyewe huko vijijini na mara
chache wanaweza kupewa pumba za mahindi, mtama, alizeti, punje chache za
mahindi au mabaki ya chakula. Kwa hiyo mlo wa
o wa kila siku wanaupata kwa
kutafuta mizoga ya wadudu pamoja na kula majani. Protini wanaipata kwa kula
wadudu kwenye majani, udongo na magome ya miti.
c)
Mwanga na joto
Kuku wa kienyeji hawapewi mwanga wa joto na hivyo kupunguza gharama za
uendeshaji wa
mradi huu wa ufugaji.
d)
Gharama za dawa na chanjo
Wafugaji wa kuku wa kienyeji kwa muda mrefu wamekuwa hawatumii dawa na
chanjo kupambana na magonjwa kwa vile kuku hawa wanavumilia sana magonjwa.
Lakini kadri ufugaji ulivyozidi kuwa na thamani na watu k
ukaa karibu karibu, kuku wa
kienyeji wakaanza kupata baadhi ya magonjwa japo si kama wa kisasa. na ugonjwa
wa kideli ndiyo unaoonyesha kuwa sumbua wafugaji wa kuku wa kienyeji. Uzuri ni
kwamba ugonjwa huu unachanjo na hivyo taratibu za uchanjaji zikifuatwa
huwa si
tatizo. Magonjwa mengine ni kama tyhoidi ya kuku, koksidiosisi, na viroboto. Hata
hivyo gharama za kupambana na haya magonjwa ni ndogo kwa hawapati mara kwa
mara. Njia zinazotumika kuzuia na kupambana na magonjwa ya kuku vijijini ni
pamoja na njia
za asili (madawa asili), na njia za kisasa (chanjo).
e)
Matatizo mengine ya kuku wa kienyeji
Ukiondoa magonjwa, ufugaji wa kuku wa kienyeji huko vijijini matatizo kama wizi,
ndege wala kuku kama mwewe, upatikanaji mgumu wa wataalamu wa mfugo, uhaba
wa ch
akula na shida ya masoko vinarudisha nyuma maendeleo ya wafugaji wa kuku.
2. Masoko
Hakuna soko lililotengwa maalumu kwa ajili ya kuuzia kuku wa kienyeji toka vijiji au
huko huko vijijini. Hata hivyo kunaongezeko kubwa sana la ulaji wa nyama na mayai
toka
kuku wa kienyeji mijini japo linalopelekea wafanyabiashara toka mijini kwenda
kufuata kuku na mayai ya kienyeji huko vijijini. Kulingana na ongezeko la uhitaji wa
kuku wa kienyeji linaoendelea kila siku, soko la kuku wa kienyeji kwa sasa si tatizo,
hata w
anaofuga hawawezi kutosheleza hitaji la soko hili huria.
3. Uboreshaji wa ufugaji wa kuku wa kienyeji
Kulinga na ongezeko la uhitaji wa kuku wa kienyeji katika soko, ipo haja ya kufanya
ufugaji wenye tija kwa kuufanyia maboresho kidogo katika maeneo ya n
yumba
wanamoishi kuku, chakula chao, matunzo kiafya, na kuingiza kuku wanaozaliana
zaidi au kuongeza thamani ya kuku wa kienyeji kwa kuchanya na aina ya kisasa.
Uzuiaji wa magonjwa unaweza kupunguza vifo vya vifaranga hadi asilimia 30.
Ulishaji wa chakula
kizuri unasaidia ufanyaji kazi mzuri wa mwili kama ukuaji, utagaji
mayai, na ubora wa nyama. Ili kukidhi mahitaji wa walaji zipo haja za kuyafanyia
utafiti madawa ya asili yanayotumika kwa kuyaboresha ili yatumike na kupunguza
matumizi ya kemikali.
KUKU
WA KISASA
1. Mtaji
Mtaji unaohitajika kuanzisha ufugaji wa kuku utategemea kwa kiasi kukubwa na
ukubwa wa shamba lako la kuku unalodhamilia kulianzisha. Ufugaji wa kuku
unamhitaji yake ya mwanzo ya uwekezaji kwa ajili ya;
a)
Ugharamikiaji wa vitu visivyoha
mishika
-
Hapa tunazungumzia vitu kama vifaa vya ujenzi wa banda na gharama za ujenzi,
vifaa vya maji ya kunywa na chakula, vifaa kwa ajili ya mwanga na joto, maeneo ya
kulala na kutagia mayai (kwa kuku wa mayai).
Banda
la kuku linatakiwa liwe na hewa ya ku
tosha lisiloweka unyevu na ukubwa
wake utategemea idadi ya kuku unaotarajia kuwafuga. Kila kuku anahitaji eneo la
mraba la kuanzia futi 1.5 hadi 1.8 wastani wa eneo za mraba 1.6, hapa jumla ya
eneo linalo hitajika litazidishwa na idadi ya kuku unaotarajia
kuwafuga.
Vifaa vya maji
-
Kuku wanahiji maji yawepo kila wakati wawapo bandani, hivyo kabla
ya kuanzisha ufugaji wa kuku hakikisha kwamba unauwezo wa kupata maji safi kwa
ajili ya kuku kila siku. Kama unatarajia kufanya ufugaji mkubwa hakikisha una
matanki
ya kuhifadhia maji kuondokana na ukosefu wa maji. Ndani ya banda weka
vifaa 4 vya kunyea maji kwa kila kuku 100 na ukubwa wa vifaa hivyo utaongezeka
kwa kadri kuku wanavyokua. Kama unatumia vifaa vinavyotoa maji vyenyewe mfano
mabomba basi sehemu mbili zi
natosha kuwanywesha kuku 100.
Vifaa vya chakula
-
Matrafu matatu kwa kila kuku 100 lazima yawekwe ndani ya
banda ili kuku waweze kula chakula kwa uhuru na si kwa kugombaniana. Kama
matrafu yakiwekwa kwa njia ya kuyaning'iniza, basi matrafu mawili kwa kila ku
ku 100
yanatosha kulisha kuku. Ukubwa wa matrafu utaongezeka kadri kuku wanavyokua.
Vifaa vya joto na mwanga
-
Joto kwa kuku ni muhimu sana hasa kuku wakiwa
katika hatua ya vifaranga ambapo hawawezi kuhimili baridi. Vifaranga wakiachwa
kwenye baridi wanaath
irika haraka na kupoteza uhai wao, hivyo joto kwao ni
muhimu hadi wafikapo zaidi ya mwezi mmoja ambapo huanza kutengeneza uwezo
wa kukabiliana na baridi. Wafugaji wadogo na hasa wale walio maeneo yasiyo na
umeme wanaweza kutumia majiko yaliyotengenezwa mah
ususi kwa utumiaji wa
mkaa kuhakikisha vifaranga wanapata joto. Lakini kwa wale walioko maeneo yenye
umeme watumie taa za umeme zenye uwezo wa kutoa mwanga na joto (balbu na
siyo tubulaiti). Kwa wale wanaotumia mkaa, basi mwanga utolewe kwa njia ya taa za
mafuta zinazo ning'inizwa kwa juu, lakini hakikisha zinatoa mwanga wa kutosha
ndani ya banda. Aidha kwa maeneo yasiyo na uhakika wa umeme taa za mafuta
ziwekwe ndani ya banda kwa tahadhari.
Stoo
-
stoo ni
muhimu kuwepo katika shamba la kuku itakayotumika kuweka vifaa,
chakula, pamoja na mayai yanaokusanywa wakiwa wameanza kutaga (kwa kuku wa
mayai). Trafu ndo za chakula na maji vinaweza kutunzwa humo kwa msimu
mwingine wa vifaranga.
b)
Matumizi ya kawaida
ya kila siku
Haya ni matumizi ya kununua vifaranga, kulipia bili za maji na umeme (kununua
mkaa, mafuta), na kununua chakula. Vifaranga wanaotakiwa ku nunuliwa ni wale
waliotoka ktotolewa (wenye umri wa siku moja) na hakikisha unawapata kutoka
kwenye shamb
a lenye uhakika wa kupambana na magonjwa. Aina ya chakula
kitategemea aina ya kuku unaowafuga (wanyama au wa mayai). Vifaranga huanza
kula mapema mara baada ya kuzaliwa na huendelea kula kadri wanavyo kua bila
kupunguza kwa muda wa miezi minne.
Chakula cha
kuku wa mayai (Layers mash)
Chakula cha mwanzo kabisa cha kuku wa mayai vifaranga) huitwa "
chiki mashi"
na
kinahitajika wapewe vifaranga hadi watakapofikisha umri wa wiki 8
-
9
.
Kiasi cha
protini katika chakula cha kifaranga wa siku moja hadi wiki 8 ni asil
imia 22
-
24.
Chakula kinachofuata ni cha kuku wanaokua na hujulikana kwa jina la "
growazi
mashi
" na waanapewa kuku hadi wanapofikisha umri wa wiki 18. Kiasi cha protini
katika chakula hiki wanachopewa kuku wa kuanzia wiki 8 hadi 18 ni asilimia 14.
Aina ya m
wisho ya chakula cha kuku wa mayai ni cha wale wanaoanza na
walikwishaanza kutaga mayai. Kuku huanza kutaga mayai wakiwa na umri wa wiki
18
-
20 na chakula cha kuku wanaotaga mayai hujulikana kwa jina la
"leyazi
mashi"
na huwa na asilimia 16
-
20 ya protini.
C
hakula cha kuku wa nyama (Broiler's mash)
Tofauti na kuku wa mayai wanaopewa chakula cha aina tatu, kuku wa nyama wao
hupewa chakula cha aina mbili kama ifuatavyo;
Wakiwa na umri wa siku moja hadi wiki nne wanapewa chakula kinachoitwa "
chiki au
broila stat
a"
chenye asilimia 22
-
24 ya protini kama ilivyo kwa vifaranga wa mayai.
Aina ya pili na ya mwisho wanapewa wanapokuwa kwenye umri wa wiki 5
-
7 ambapo
uuzaji unaanza wanapewa chakula kinachoitwa broila finisha chenye asilimia 19
-
20
ya protini.
Gharama nyingi
ne
Gharama nyingine za ufugaji wa kuku zitatokana na ununuzi wa chanjo pamoja na
madawa ya kuwafanya kuku waendelee kuwa na afya na kuleta matunda ya
kuridhisha kwa kukinga na kupambana na magonjwa ya kuku. Aina ya dawa na
njanjo za kutumia unahitaji kupa
ta ushauri kutoka kwa daktari wa mifugo aliyekaribu
nawe. Pia matengenezo na marekebisho ya hapa na pale yatahitaji pesa pamoja na
kuwalipa wafanyakazi wanao kusaidia kazi kwenye shamba lako la kuku. Lakini pia
gharama nyingine za dharula zaweza kujitokeza
, hivyo ni vema kuweka katika bajeti
yako.
2. Eneo la kufugia na uchaguzi
Eneo la kufugia ni kitu muhinu sana cha kuzingatia wakati unapofanya uamuzi wa
kutaka kufuga kuku. Wakati wa kuchagua eneo hilo vigezo vifuatavyo ni veme
vikazingatiwa
i) Eneo liwe
na nafasi ya kutosha tena ikiwezekana liwe kwenye mwinuko ili kurushu
hewa ya kutosha.
ii) Eneo lisiwe karibu sana
na makazi ya watu lakini kuweko na njia za mawasiliano
hasa barabara ili kuruhusu uingizaji wa chakula na usafirishaji wa mayai na kuku
kwenda sokoni.
iii) Eneo liwe na upatikanaji wa maji safi na umeme wa uhakika
iv) Eneo lisiwe na
wadudu au wanyama waharibifu kwaa kuku au vifaranga
v) Epuka kuchanganya aina tofautitofauti za ndege kupunguza maambukizano ya
magonjwa.
3. Usimamizi katika ufugaji wa kuku
Hii ni sehemu ya muhimu sana katika mradi wa ufugaji wa kuku kama ilivyo kwa
mra
di wowote kwani bila umakini katika usimamiaji mradi utakufa au hautaleta
matunda yaliyotarajiwa. mambo ya msingi ya kusimamia ili ufugaji uwe na tija ni
pamoja na chakula, udhibiti wa magonjwa, na udhibiti wa watu wanaoingia ndani ya
shamba au banda lako.
Chakula lazima kisimamiwe kwa uangalifu ili kupunguza
upotevu lakini pia kuwa na hakika kuwa kuku wako wanapata chakula kinacho stahili
na kwa wakati ili waweze kuku vema na kutaga mayai mengi.
Kuku wapewe
chakula nusu ya chombo wanachotumia na kisha nus
u nyingine baadaye ili kuepuka
wasije wakakimwaga kama tabia yao ilivyo, lakini pia kuku hula vizuri chakula kikiwa
hakijakaa muda mrefu
ndani ya chombo.
Kuku wa kisasa hushambuliwa na magonjwa mengi, lakini mengi yanatokana na
uchafu ndani ya banda. Maa
mbukizi haya
yanaweza kutokana na vyombo vichafu
vya maji ya kunywa, chakula chenye wadudu waliotokana na kunyesi cha kuku. Ili
kuzuia kuku kunyea chakula ni vema kuning'iniza vyombo vya chakula ili kuku
asiweze kupanda akiwa anakula chakula na kuchafua c
hakula. Unyevuunyevu ndani
ya banda lazima uepukwe ili kupunguza maambukizi ya magonjwa ya mapafu na
uzalianaji wa vimelea vya magonjwa.Baadhi ya magonjwa yanashambulia kuku ni
pamoja na Koksidiosisi, ugonjwa wa Mareksi, Gumboro, Kideli, Taifodi ya kuku, n
dui
na minyoo.
Ni vema kumtafuta daktari wa mifugo aliyekaribu nawe kwa ushauri wa
na namna ya kukabiliana na magonjwa haya kwa kuku wako tena hata kabla ya
kuanza ufugaji.
4. Masoko
Kazi ya kutafuta masoko inatakiwa kufanyika hata kabla ya wakati wa uu
zaji wa kuku
au mayai kufika. Tena ni vema kujiridhisha hata kabla ya kuanza kufuga kama
masoko yapo na ni wapi na utayafikiaje. Hii itakurahisishia wakati ukifika unakuwa
hupati shida yeyote ile. Mambo yafuatayo lazima uyazingatie wakati unatafuta soko
la
kuku au mayai;
i) Biashara yako lazima iwe karibu na masoko ya kuku au lazima kuwe na urahisi wa
kufika kwenye masoko ya kuku (yawepo mawasiliano ya barabara).
ii) Biashara ya aina gani unataka kufanya, mayai au kuku, wazima (hai) au
waliochinjwa na kuten
genezwa.
iii) Lazima ujue bei ya aina ya bidhaa kabla ya kuipeleka sokoni (siku hizi simu za
mkononi zimerahisiha mawasiliano)
iv) Fanya matangazo ya biashara yako kabla ya kuanza kuuza ili watu wajue, tene ni
vema ukaanza matangazo mapema kabisa ikurahisi
shie kupata masoko.
5. Utunzaji wa kumbukumbu
Mali bila daftari huisha bila kujua, ni vema kutunza kumbukumbu ya mambo yote ya
muhimu yanayofanyika ndani ya shamba lako la mifugo. Mbali na kumbukumbu
nyingine, mambo yafuatayo lazima yawekewe kumbukumbu;
namba ya kuku ulionao
kwa umri wao, kumbukumbu ya chakula, tarehe za matibau na chanjo,
tarehe za
kuja daktari wa mifugo, kumbukumbu za vifo, mayai yaliyotagwa, mauzo ya mayai
au kuku, gharama za maji na umeme na gharama za wafanyakazi. Hii itasaidia kujua
kama kuna faida au hasara inayotokana na ufugaji wako wa kuku. Hivy ni muhimu
kufanya mahesabu ya mapato na matumizi kila baada ya muda fulani hasa kila
mwaka ili ujue kama kuna hasara inatokana na nini uirekebishe.
Share this article :

Chapisha Maoni

 
Copyright © 2013. KCC KIBAHA - All Rights Reserved
Template Created by KIJANA WA LEO Published by TITUS KAPOMA
Proudly powered by Blogger