Chotara wanatokanana na majogoo wekundu ni wakubwa na majogoo yake pia ni wakubwa kama wanavyoonekana hapa kwenye picha
Chotara wekundu(Rhode Island Red): kuku hawa ni wazito (Heavy breed) wanafaa kwa mayai na nyama (dual purpose) na pia majogoo yake ni mazuri kwa kuzalishaji kama ukichanganya (cross breed) na kuku wa asili au mbegu nyingine yoyote ile utakuwa umeboresha mbegu yako kupata kuku wakubwa na wenye uzito. wanauwezo mkubwa wa kuhimili magonjwa kwa kiasi kikubwa na wanataga mayai kwa wingi,majogoo yana wastani wa kilo 4 hadi kilo 6 nyama yake.
FAIDA nyingine kwa hawa kuku wekundu ni wazuri kwa biashara ya nyama, baada ya miezi minne unaweza kuwauza kuanzia Tshs. 15,000/= kama nyama kwa sababu wanawahi sana kupata uzito.wanapofikia miezi sita/saba unaweza kuuza kwa bei ya Tshs.25,000/= hadi 30,000/= kama ukichukuwa vifaranga hawa na ukabahatika kupata majogoo 50 hadi 100 na kuwauza kwa bei kati ya 25,000/= hadi 30,000/= utakuwa umepata faida kubwa sana.kwa hiyo unaweza kuwatumia kama nyama au mayai vyote vinalipa.
KUCHI
Baada ya muda si mrefu tutaanza kuuza vifaranga wa kuchi huyu hapa chini kwa sasa tunandaa kuku wazazi
Kuchi chotara wekundu : Hawa ni kuchi chotara wekundu siza zake hapati magonjwa kama kuku wengine na ni watagaji wazuri pia.karibu kuwa mfugaji utafurahia mifugo yako.unakula shambani mwako mazao mazuri ujivunie.
Black Australorp (Weusi/Malawi) ; ni kuku weusi na wenye maumbo makubwa kama wanavyoonekana kwenye picha.sifa ya kuku hawa ni watagaji sana kuliko kuku mwingine yoyote.mayai yake ni madogo kuliko kuku wengine,siyo mzito kama kuku wengine lakini watagaji wazuri.
Barred Plymouth Rocks: kuku hawa ni wazuri wanafaa kwa mayai na nyama (dual purpose) ana rangi kama ya kanga.
Ni mtagaji mzuri na hashambuliwi na magonjwa.
Chapisha Maoni