Ushauri :
Tunashauri jamii kufuga kuku wa kuchanganya damu (cross breed) yaani pandisha kuku wa kienyeji na wale wa kisasa (indigenous + Pure breeds) ili kuweza kupata kuku ambao kwa kiasi fulani huhimili magonjwa
Tunatoa ushauri kwa wateja wetu bure kuhusu mbegu gani anunue na jinsi ya kuwahudumia tangu anapowanunua hadi wanapoanza kutaga na kuendelea.ikiwa ni kwa upande wa madawa na chakula pamoja viwango vya kuwalisha.wateja wengi wanakosea sana taratibu za kuwalisha kuku kitu ambacho kinawapa hasara lakini kama akiwa ni mtu wa kuzingatia anaepukana na magonjwa yanayoweza kujitokeza kutokana na uzembe wake.
Chakula nalo ni tatizo watu wengi wanakosea vipimo, kuku anayetaga anatakiwa ale kwa kiwango maalum kinachotakiwa.kuku akila na kupitiliza kiwango au kupunguza hatagi kwa kiwango kinachotakiwa au asitage sana itategemea ameathirika kwa kiwango gani kwa sababu akiwa na mafuta kwa wingi hatagi,akipungukiwa na chakula hatagi.
Minyoo na utitiri nalo ni tatizo linachangia kuku kutokutaga, unashauriwa kumpa kuku dawa za minyoo na utitiri kwa wakati.
Tunashauri kutumia mabanda ya ghorofa kwa ajili ya vifaranga ili kuepukana na bacteria wanatokana maranda kwetu utajionea na ni faida kwako.
Wasiliana nasi upate mbegu bora na ambazo hujawahi kuwa nazo ili kujikwamua katika hali ya umaskini.
MAGONJWA YANAYOSABABISHWA NA VIRUSI
1. Mdondo (Newcastle):
Dalili zake:
kuku kukohoa,kuhema kwa shida,kutokwa na ute mdomoni na puani,hupatwa na kizunguzungu, kuharrisha mharo wa kijani na manjano na hatimaye kuku hufa ghafla. Vifo huweza kufikia asilimia90
2. NDUI YA KUKU: Fowlpox)
Kuku hupatwa na vipele vya mviringo kwenye upanga, (masikio,miguu na sehemu zisizo na manyoya.vifo vichache kwa kuku wakubwa, wadogo huweza kufa nusu ya kundi.CHANJO WIKI YA NANE
(wapewe antibiotic na vitamini) hakuna tiba)
3. MAHEPE (.Marek's disease)
Kuku kupooza miguu, mabawa na shingo huweza kupinda, mara nyingi huwapata kuku wenye umri wa wiki ya 16 hadi 30.kiasi cha robo ya mitemba wanaweza kufa.
(chanja vifaranga wakiwa na umri wa siku moja)
4. GUMBORO :
vifaranga huharisha mharo mweupe,huhangaikahangaika, hushindwa kuhema, manyoya husimama, hudumaa, hutetemeka na hatimaye hufa.vifo vyaweza kufikia 5% hadi 10%.
(Hakuna tiba wapatiwe chanjo ya gumburo)
5. MAGONJWA YASHAMBULIAYO MFUMO WA HEWA
(Infectious bronchitis, laryngotracheitis or chicken influenza)
upungufu wa mayai kwa kuku wanaotaga,vifaranga hupata matatizo ya kupumua na kupiga chafya na hufa kwa wingi
(huzuiwa kwa chanjo) hakuna tiba.)
6. MAFUA MAKALI YA NDEGE:
kupumua kwa shida, kukohoa na kupiga chafya, sehemu za kikole(kidevu na kishungi) hubadilika na kuwa rangi ya zambarau,kutokwa na machozi,kupinda shingo na kuanza kuzunguka, kuvimba kichwa, kuharisha kinyesi chenye majimaji, rangi ya kijani na baadaye kinyesi cheupe.
(hakuna tiba muone daktari
Je unazijua aina za kuku wa kienyeji?
Kuku wa kienyeji /kizungu
UFUGAJI WA KUKU WA ASILI NA WAKISASA USHAURI BURE KUTOKA KCC KIBAHA-PWANI
7. HOMA YA MATUMBO: (Salmonella gallinarum)
ugonjwa huu unaweza kurithiwa kupitia kwenye mayai au kuambukizwa kutokana na kuku wagonjwa, kinyesi, kudonoana, na mazingira machafu,
Kuku huharisha mharo wa kijani, vilemba na upanga hupauka kutokana na upungufu wa damu, manyoya husimama.vifo huweza kufikia 50%.
Weka banda katika hali ya usafi,ondoa kuku waliougua,usitumie mayai yenye ugonjwa kuangulia.
8. Pullorum bacillary white diarrhea (bacteria salmonella pullorum)
huathiri zaidi vifaranga(kabla ya umri wa wiki 4) vifaranga hujikusanya pamoja na kutetemeka kama waliopatwa na baridi.huharisha mharo mweupe hamu ya kula hupungua,manyoa hunyea na hupumua kwa taabu.vifo huweza kufikia asilimia 50.
9. kipindupindu cha kuku(Fowl cholera)
kuku kuhara mharo wa rangi ya njano.husinzia na kulegea,hulala kichwa kikining'inia kwenye mabawa.manyoya husimama,kuhema kwa shida,hushindwa kusimama na hatimaye hufa.vifo huweza kufikia asilimia 50
Usafi wa banda(huweza kutibika kwa dawa ya sulfa)
10.Ugonjwa unaoshambulia mfumo wa hewa (chronic respiratory)
Kuku kupata mafua, kukohoa kushindwa kupumua, kutokwa na makamasi,vifaranga hudumaa,utagaji hupungua na viungo vya mifupa huweza kuvimba
Tiba: antibiotic hutibu,usafi wa banda.
11. UGONJWA WA KUHARA DAMU:
Kuku huharisha kinyesi kilichochanganyika na damu na mara nyingine damu tupu,hudhoofisha kuku, huteremsha mabawa na hatimaye kuku huweza kufa.
Usafi wa banda,hutibiwa kwa kutumia dawa kama vile Amprolium.salfa na Esb3.Muone daktar.i
Chapisha Maoni