Jumanne, 11 Juni 20130 comments

1
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Mwongozo kwa mfugaji
BIASHARA YA UFUGAJI BORA
WA KUKU WA ASILI
KItABU cHA MWOnGOzO2
Biashara ya kuku wa asili
RLDc na Uboreshaji wa Maisha Vijijini
Shirika la Rural Livelihood Development Company (RLDC ni moja ya mafanikio
ya ushirikaiano kati ya Tanzania na Uswisi kwenye mchakato wa kupambana na
umaskini na kuboresha maisha ya jamii za vijijini. Hii ni taasisi isiyo ya kibiashara
ili yoanzishwa mwaka 2005 na mashirika ya Intercooperation na Swisscontact,
lengo kuu likiwa kutekeleza Programu ya kuendeleza maisha ya jamii za vijijini
(RLDP). Programu hii inasha bihiana na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupambana
na Umaskini (MKUKUTA). Dhamira kuu ya RLDC ni Kuendeleza/kuboresha mifu
mo ya masoko ili kuwawezesha wazalishaji wa vijijini kutumia
fursa zilipo kuboresha maisha yao.
Kwa sasa, RLDC inatelekeleza awamu ya pili ya mpango wake (2008-2011)
na inaweka msukumo zaidi kwenye uendelezaji wa mifumo ya masoko. RLDC
inafanya kazi katika mikoa sita ya Kanda ya kati-Dodoma, Singida, Morogoro,
Shinyanga, Tabora, na Manyara. Jamii nyingi maskini zinaishi katika ukanda huu
wenye sehemu kubwa yenye hali ya mvua chache na nusu jangwa inayostawisha
shughuli chache za kiuchumi.
Hata hivyo kuna fursa nyingi sana zinazoweza kutoa ajira na kuboresha ya
jamii zake. RLDC inafadhiliwa na Serikali ya Uswisi kupitia shirika la Uswisi la
maendeleo (SDC).
Kwa sasa RLDC inawezesha sekta za pamba, alizeti, maziwa, ufugaji wa kuku wa
kienyeji, mpunga na habari kupitia vipindi vya redio kwa ajili ya wazalishaji wa
vijijini.
“RLDc inaboresha mifumo ya masoko ili kuwezesha wazalishaji wa
vijijini kuinua maisha yao”BIASHARA YA UFUGAJI
BORA WA KUKU WA ASILI
MWOnGOzOii
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
YALIYOMO
Utangulizi 1
Sehemu ya Kwanza 2
Njia tofauti za kufuga kuku
Sehemu ya Pili 5
Banda la Kuku: Sifa za banda bora la Kuku
Sehemu ya Tatu 9
Kuzaliana na kutotolesha : Uchaguzi wa Kuku bora
Sehemu ya Nne 13
Utunzaji wa Kuku
Sehemu ya Tano 16
Magonjwa ya Kuku
Sehemu ya Sita 19
Kusimamia Ufugaji Wako: Kutunza kumbukumbu
Sehemu ya Saba 22
Masoko
Sehemu ya Nane 24
Chama cha Akiba na Kukopa 1
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Utangulizi
Tanzania ina idadi ya kuku wa kienyeji wanaokadiriwa kuwa million 34 ambao wanafugwa
kwa mtindo wa huria. Ufugaji wa aina hii hufanyika vijijini na mijini pia.
Idadi hii ya kuku bado ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji halisi ya Watanzania
wanaokadiriwa kuwa milioni 40 (sensa ya mwakaxxx). Ulaji wa nyama ya kuku nchini
unakadiriwa kuwa ni wastani wa kilo 0.7 kwa kila mtu kwa mwaka mzima ilihali Shirika
la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linakadiria wastani mzuri wa ulaji wa
nyama kuwa ni kilo 6.8 kwa mtu kwa mwaka. Hii inaashiria kuwa soko la kuku nchini ni
kubwa, ambayo ni fursa muhimu kwa wafugaji wa kuku.
Ufugaji wa kuku ni nyenzo nzuri ya kujipatia kipato katika kaya kwa sababu ufugaji wa
kuku hauhitaji mtaji mkubwa na hauna kazi kubwa kiuendeshaji. Katika ufugaji huria kuku
hujitafutia chakula wenyewe. Pia inapowezekana hupewa mabaki ya chakula, chenga,
pumba au nafaka yoyote inayopatikana katika mazingira husika. Kwa walio wengi ifikapo
nyakati za jioni, kuku hulala jikoni au ndani nyumbani kwa mfugaji mwenyewe. Ufugaji
huu ni rahisi kwa kuwa hauna gharama kubwa ila faida yake ni kitoweo tu au fedha
kidogo sana.
Kutokana na lishe duni na kuzaana wenyewe kwa wenyewe (bila kubadili jogoo), kuku
wa kienyeji walio wengi wana uzito mdogo. Wana wastani wa uzito wa robo tatu za kilo
hadi kilo moja wakiwa na umri wa zaidi ya mwaka mmoja. Ila wakitunzwa vizuri zaidi na
kuboreshwa wana uwezo wa kufikia uzito wa kilo moja hadi moja na nusu katika umri
wa miezi sita hadi nane.
Kwa upande wa utagaji wa mayai kuku wa kienyeji kwa wastani hutaga mayai 50 hadi
65 kwa mwaka. Wakitunzwa vizuri zaidi huweza kufikia uzalishaji wa mayai 80 hadi 100
kwa mwaka.
Kijitabu hiki kinatoa maelezo ya njia na kanuni mbalimbali rahisi za kuzingatia ili mfugaji
aweze kuzitumia kupata mazao mengi na bora zaidi yatakayomnufaisha kimapato na
kwa matumizi mengine. Kanuni hizi ni pamoja na:
√ Kuchagua njia bora ya kufuga na sifa za mabanda bora ya kuku
√ Kuchagua aina bora ya kuku wa kufuga, kuzaliana na kutotolesha
√ Utunzaji wa vifaranga
√ Kutengeneza chakula bora cha kuku
√ Kudhibiti na kutibu magonjwa
√ Kutunza kumbukumbu
√ Kutafuta masoko
12
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Sehemu ya Kwanza
Njia tofauti za kufuga kuku
Mambo yanayomfanya mfugaji kuamua atumie njia fulani ya kufuga ni pamoja na uwezo
wa kugharamia shughuli ya ufugaji wa kuku na ukubwa wa eneo alilonalo la kufugia.
Katika sehemu hii utajifunza njia tatu za kufuga kuku ambazo ni:
1. Kufuga huria
Kuku huachwa wenyewe kujitafutia chakula na
maji. Njia hii inatumika zaidi kufuga kuku wa
kienyeji. Mara chache sana mfugaji huwapatia
kuku chakula cha ziada. Kwa ufugaji huu lazima
kuwe na eneo kubwa la kutosha kuku kuzunguka
na kutafuta chakula. Kuku hulala eneo lisilo rasmi
kama vile jikoni, kwenye kiambata n.k.
Faida zake
• Ni njia rahisi ya kufuga.
• Gharama yake pia ni ndogo.
• Kuku wanapata mazoezi ya kutosha.
• Kuku wanapata chakula mchanganyiko ambacho kinafaa kiafya.
Hasara zake
• Kuku huwa hatarini kuibiwa au kudhurika na wanyama wakali na hali mbaya ya hewa.
• Ukuaji wa kuku ni hafifu, hufikia uzito wa kilo 1.2 baada ya mwaka.
• Huharibu mazingira kama kula na mimea ya
bustanini mazao kama nafaka.
• Ni rahisi kuambukizwa magonjwa.
2. Kufuga nusu ndani – nusu nje
Huu ni mtindo wa kufuga ambapo kuku wanakuwa
na banda lililounganishwana uzio kwa upande
wa mbele. Hapa kuku wanaweza kushinda ndani
ya banda au nje ya banda wakiwa ndani ya uzio.
Ufugaji huria
Ufugaji wa nusu ndani na nusu nje3
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Wakati wa mchana kuku huwa huru kushinda ndani ya banda hasa wanapotaka kutaga
na wakati wa kuatamia au wanaweza kukaa ndani ya uzio nje.
Faida za kufuga nusu ndani na nusu nje
• Kuku wanakuwa salama mbali na maadui mbali mbali.
• Utaweza kuwalisha kuku wako vizuri hivyo wataweza kuongeza uzalishaji wa mayai
na wa nyama (kwa kukua haraka).
• Itakuwa rahisi kwako kudhibiti wadudu na vimelea vinavyoweza kuleta magonjwa kwa
kuku wako.
• Ni rahisi kuwatenganisha kuku katika makundi tofauti na kuwahudumia ipasavyo.
• Ni rahisi kutambua kuku wagonjwa kuliko kufuga huria.
• Kuku watapata mwanga wa jua wa kutosha pamoja na hewa safi.Wakati wa jua kali
watakuwa huru kuingia ndani ya banda na kukaa kivulini.
• Kuku hawatafanya huharibifu wa mazao yako shambani au bustanini na kwa majirani
zako.
• Utapata urahisi wa kukusanya na kupeleka mbolea bustanini au shambani.
Changamoto ya kufuga nusu ndani na nusu nje
• Huna budi uwe na muda wa kutosha kwa ajili ya kuwahudumia kuku wako.
• Pia utahitaji kuwa na eneo kubwa kiasi la kufugia.
• Pia utaingia gharama ya ziada kidogo ya kutengeneza banda na wigo na kuwapatia
uku chakula cha ziada.
• Hata hivyo gharama za muda huo na za vifaa vingine zitafidiwa na mapato ya ziada
utakayopata kwa kufuga kwa njia hii.
3. Kufuga ndani ya Banda tu
Njia nyingine ni kuwafuga kuku ndani tu. Katika njia hii, kuku hukaa ndani wakati wote.
Njia hii ya ufugaji utumiwa zaidi na wafugaji wa kuku wa kisasa. Lakini yaweza kutumika
hata kwa kuku wa asili hasa katika sehemu zenye ufinyu wa maeneo.
Changamoto za ufugaji wa ndani ya banda tu
• Unatakiwa uwe na muda wa kutosha wa kuwahudumia kuku wako kikamilifu.
• Pia unatakiwa kuwa na mtaji mkubwa wa kujenga banda na kuwanunulia kuku chakula.
• Ugonjwa ukiingia na rahisi kuambukizana.Vilevile kuku huweza kuanza tabia mbaya
kama kudonoana, n.k. 4
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Faida za kufuga ndani tu
• Ni rahisi kutambua na kudhibiti magonjwa.
• Ni rahisi kudhibiti upotevu wa kuku, mayai na vifaranga.
• Ni rahisi kuwapatia chakula kulingana na mahitaji ya kila kundi.
• Ni rahisi kuwatambua na kuwaondoa kuku wasiozalisha katika kundi.
Ni ufugaji upi unafaa zaidi kutumika kwenye mazingira ya vijijini?
Kwa ujumla, njia rahisi na inayopendekezwa kutumiwa na mfugaji wa kawaida kijijini
ni ya ufugaji wa nusu ndani na nusu nje, yaani nusu huria. Hii inatokana na faida zake
kama zilizoainishwa hapo awali. Kwa kutumia mfumo huu wa ufugaji, utaepuka hasara
za kufuga kwa mtindo wa huria kama zilivyainishwa mwanzoni mwa sehemu hii ya
kitabu hiki.
Pia ukitumia mtindo wa ufugaji wa nusu huria utafanya ufugaji wako kwa njia bora
zaidi ndani ya uwezo ulionao, kwa sababu kwa sehemu kubwa utatumia mali ghafi
inayopatikana katika eneo lako. 5
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Sehemu ya Pili
Banda la Kuku
Sifa za banda bora la Kuku
Ukiamua kufuga katika banda kwa njia mbili zilizoelezwa awali utatakiwa kujenga banda
lenye sifa zitakazokidhi mahitaji ya msingi ya kuku. Banda bora la kuku linatakiwa kuwa
kama ifuatavyo:
Liwe jengo imara
• Pasiwe na sehemu zilizo wazi kwenye msingi na kati ya ukuta na paa.
• Banda lijengwe na vifaa vinavyopatikana katika mazingira yako ili liwe na gharama
utakayoweza kumudu.
• Unaweza kutumia matofali ya udongo, udongo, miti, fito,n.k. Ukitumia fito au mabanzi
ondoa maganda ili kuthibiti mchwa.
• Jengo mara litazuia maadui kama panya, vicheche, paka, nyoka na wezi kuingia ndani
ya banda na kuwadhuru au kuwaiba kuku.
Liwe rahisi kusafisha
• Kuta na sakafu visiribwe zisiwe na nyufa ili kurahisisha kusafisha.
• Pia itadhibiti kusiwe na wadudu wa kujificha katika nyufa kama papasi, viroboto n.k.
• Sakafu ya banda lazima iwekewe matandazo kama pumba ya mpunga au maranda
ya mbao au mabaki ya mazao au nyasi kavu kutegemeana na kinachopatikana kwa
urahisi katika mazingira yako.
• Matandazo haya husaidia kunyonya unyevu unaotokana na kinyesi cha kuku au maji
yanayomwagika katika banda.
• Banda hubakia kavu bila kuwa na harufu mbaya na wadudu kama inzi hata vimelea
vya magonjwa hudhibitiwa.
Eneo la nje kuzunguka banda kuwe na usafi wa kudumu
Hali ya usafi nje ya banda itafanya wadudu kama siafu au mchwa na wanyama kama
panya na paka mwitu wakose maficho. Nje ya banda ndani ya uzio kuwe na miti midogo
na mimea mingine midogo kwa ajili ya kivuli. 6
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Ufugaji nusu huria
Liwe na nafasi ya kutosha kwa kuku waliopo:
Kwa kawaida eneo la mita mraba moja hutosha
kuku wanne wanaotaga au kuku 8 wa nyama.
Nafasi ya mita mraba 1 inatosha vifaranga 16
hadi kufikia umri wa majuma manne.
Liweze kuingiza hewa na mwanga wa
kutosha: Banda linaloweza kuingiza hewa
safi na kutoka ndani yake hubaki kavu. Harufu
mbaya hutoka na kuku huweza kupumua hewa
safi. Hii husaidia pia kudhibiti kuzaliana kwa
vimelea vinavyosababisha magonjwa,hivyo
hudhibiti magonjwa.
Lisiwe na joto sana au baridi sana: Panda miti ya kuzunguka banda lako ili eneo liwe
na kivuli cha kutosha na pia lisiwe na upepo mkali.Kama hali halisi ya eneo la kufugia ina
joto kubwa kwa vipindi virefu paa la banda wakati wa ujenzi liinuliwe juu zaidi kuruhusu
mzunguko zaidi wa hewa na joto la paa ( kama ni la bati) liwe mbali juu ya kuku.
Joto kwenye banda linaweza kusababishwa na msongamano wa kuku, hivyo mfugaji
aangalie aweke idadi ya kuku inayowiana na ukubwa wa banda lake.
Paa
Liwe imara na lisilovuja. Waweza kutumia mabati,
nyasi, madebe, makuti n.k. kutegemeana na
upatikanaji wa vifaa vya kuezekea.Wakati wa
kuezeka paa lisiishie karibu sana na ukuta bali
liwe na sehemu kubwa iliyozidi ukuta kuzuia
mvua kuingia ndani kama ni ya upepo ( angalia
mchoro hapa chini).
Vifaa vinavyohitajika katika banda la kuku
Kuku wakifugwa kwa mtindo wa nusu ndani na nusu nje wanahitaji huduma mbalimbali
ndani ya banda na ndani ya wigo. Ili kutoa huduma hizi vifaa vifuatavyo ni muhimu viwe
katika banda:
Ufugaji wa nusu huria
Paa lifunike ukuta kwa sehemu kubwa7
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Vyombo vya Maji
Kuna njia nyingi za kutengeneza
vyombo vya kuwekea maji ya
kuku ya kunywa.
• Aina ya mojawapo
unayoweza kutumia
ndoo au debe la lita kumi
au ishirini ya plastiki. Kata
ndoo hiyo pande nne
kutoa nafasi ya kuku ya
kunywea kama kielelezo
kinavyoonyesha. Tengeneza idadi ya vyombo hivi inayowiana na wingi wa kuku
ulionao.
• Au waweza kutumia sufuria au beseni pana kiasi. Hii huwekewa tofali au jiwe safi
pana baada ya kuwekewa maji ya kunywa ili kuzuia kuku wadogo wasizame na maji
yasichafi liwe kirahisi.
• Vifaa maalum vya kunyweshea kuku vinapatikana katika maduka ya pembejeo za
kilimo.
Vyombo vya Chakula
Vyombo hivi ni muhimu viwe vimetengenezwa
vizuri ili visiwe chanzo cha upoteaji wa chakula.
Unapotengeneza kilishio cha kuku kumbuka
kuwa kuku wana tabia ya kuchakura. Husambaza
au kupekua chakula kwa miguu hata kwa midomo
ili kupata chakula cha chini.
Tabia hii husababisha kumwagwa kwa chakula kingi chini na kusababisha hasara.
Unaweza kudhibiti tatizo hili kwa kutengeneza vyombo visivyoruhusu kuku kuchakura
kama inavyoonyeshwa kwenye kielelezo hapa chini.
Unaweza kutengeneza kilishio hiki wewe mwenyewe au fundi seremala waliopo katika
eneo unaloishi. Inafaa kilishio kiwe chembamba ili kuku wasiweze kuingia. Pia kinatakiwa
kiwe kirefu ili kuku waweze kula bila kusongamana.
Viota
Zipo aina tofauti za viota ambazo hutumika kwa ajili ya kutagia. Ipo aina ya ambayo ni
ya kutagia kuku mmoja mmoja. Vipimo vinavyopendekezwa kwa kila kiota ni upana wa
sentimita 30, urefu sentimita 30 na kina sentimita 35. Upande wa mbele uachwe wazi
Kilishio
 Kinywesheo cha kujitengenezea Kinywesheo8
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
ila sentimita 10 za kwanza kutoka chini zizibwe na ubao
( angalia kielelezo). Weka idadi ya viota inayotosheleza
kuku ulio nao.
Pia ipo aina nyingine inayoweza kutumiwa na kuku
zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Ni kama kiota
kimoja kilichogawanywa katika vyumba kadhaa. Ila
kila chumba kina vipimo kama vya kiota kimoja(
angalia picha hapa chini).Aina hii ya kiota ina upana
wa sentimita 30 na kina sentimeta 35 na urefu wake
unategemea idadi ya viota.
Viota vinatakiwa kuwa na giza ili kuku wasiogope kuingia kutaga ndani yake. Pia giza
husaidia kupunguza tabia ya kuku kula mayai na kudonoana. Kiota kinafaa kuwekwa
mahali ambako ni rahisi kuku kuingia na kutoka. Vile vile iwe ni sehemu itakayorahisisha
usafishaji wa kiota chenyewe.
Vichanja
Kuku wana asili ya kupenda kulala au kupumzika sehemu iliyoinuka. Hivyo ndani ya
banda weka vichanja vitakavyotosheleza idadi ya kuku waliopo.
Muunganiko wa Viota
Vichanja 9
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Sehemu ya Tatu
Kuzaliana na kutotolesha
Uchaguzi wa Kuku bora
Ili upate kundi lenye kuku bora huna budi uchague jogoo bora na matetea bora wa
kuzalisha kundi lako.
Angalia sifa zifuatazo unapochagua:
• Tetea na jogoo wawe na umbo kubwa.
• Wanaokua haraka.
• Wenye uwezo wa kustahimili magonjwa.
• Matetea wanaoweza kutaga mayai mengi.
• Matetea wanaweza kuatamia na hatimaye kutotoa vifarangakwa wingi na kuvilea.
• Jogoo unaowachagua kwa ajili ya matetea au makoo yako wasiwe na uhusiano wa
damu.
Ukiishachagua wazazi wa kundi lako changanya jogoo na matetea kwa uwiano wa
jogoo mmoja kwa matetea 10 hadi 12. Ukiwa na matetea 20 utahitaji kuwa na jogoo
wawili.
o Nchini kwetu zipo aina tofauti za kuku wa asili ambao wana sifa tofauti. Wafugaji
wengi hufuga kutegemeana na uwezo wa kuku kuhimili magonjwa ,kuwa na uzito
mkubwa, utagaji wa mayai mengi n.k. Koo za kuku wa asili wenye sifa za namna hii
ni aina ya Bukini , Kuchi, Kuchere na wa Kawaida wasio na ukoo maalum. Hawa kwa
ujumla wao wakitunzwa vizuri wana uwezo wa kufanya vyema katika mazingira ya ya
nchi hii kwa sababu wameishayazoea.
Kuatamia na kuangua mayai:
Baada ya jogoo kupanda matetea au makoo, hawa watataga mayai. Mayai yanaweza
kutotoleshwa kwa njia ya asili au kwa kutumia vifaa vya kutotolesha.
Kutotoa kwa njia ya asili 10
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Hii inafanyika kwa kuku kuatamia mayai kwa hatua zifuatazo.
Kuandaa kiota:
• Kiota kiandaliwe kabla kuku hajaanza kutaga kwa kukiwekea nyasi kavu na kuzisambaza
kwa kutengeneza muundo wa kata au sahani iliyozama kidogo.
• Kiota kinyunyiziwe dawa ya unga kuua wadudu kabla na baada ya kuweka nyasi. Iwapo
kuku atajiandalia kiota chake mahali panapofaa aachwe hapo ila kiota kiwekewe dawa
ya kudhibiti wadudu.
Maandalizi ya kuku anayetaka kuatamia
Dalili za kuku anayetaka kuatamia ni:
o Anatoa sauti ya kuatamia.
o Ushungi wake umesinyaa.
o Hapendi kuondoka kwenye kiota.
o Hupenda kujikusanyia mayai mengi
Kuku wenye dalili za kutaka kuanza kuatamia
akaguliwe ili kuhakikisha kuwa hawana wadudu
kama utitiri, chawa, viroboto n.k. wanaoweza
kumsumbua wakati wa kuatamia. Akiwa na
wadudu watamsumbua hataweza kutulia
kwenye kiota na kuatamia vizuri. Matokeo yake ataangua vifaranga wachache. Hivyo
walio na wadudu wanyunyizie dawa ya unga kabla hawajaanza kuatamia ili kudhibiti
tatizo hili.
Kuatamia
Kuku anapotaga mayai yaondolewe na kubakiza moja kwenye kiota ili kumwita kuku
kuendelea kutaga. Kuku akiwa tayari kuatamia awekewe mayai kwa kuatamia. Kwa
kawaida kuku mmoja anaweza kuatamia vizuri mayai 10 hadi 13 kwa wakati mmoja.
Kipindi cha kuangua mayai ni kuanzia siku 20 baada ya kuatamia. Ukitaka kutotolesha
vifaranga wengi kwa wakati mmoja, kuku akianza kutaga yakusaye mayai yake na
kumbakizia yai moja ili aendelee kutaga.Mayai utakayokusanya yaweke mahali pasipo
na mwanga mwingi na penye ubaridi kiasi.
Fanya hivi kwa kuku kadhaa wanaotaga ndani ya muda unaokaribiana. Kila
atakayeonyesha dalili ya kuanza kuatamia muwekee mayai kati ya 10 na 12 aatamie.
Kwa njia hii wataatamia na kuangua ndani ya kipindi kimoja. Na utapata vifaranga wengi
wa umri mmoja hatimaye kuuza kuku wengi kwa pamoja.
Ufugaji wa nusu huria11
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Kulea Vifaranga
Baada ya vifaranga kutotolewa waache na
mama yao mahali penye usalama kwa muda
wa mwezi moja mbali na mwewe, vicheche,
paka, kenge, n.k. Hakikisha wanapata maji na
chakula cha kutosha muda wote.
Kulea vifaranga kwa kumtumia kuku
Njia nyingine ni kuwaweka vifaranga mahali
pazuri na kuwafunika na tenga ili kuzuia
mwewe wakati wa mchana kwa kuhakikisha
kuwa hawapigwi na jua wala kunyeshewa
mvua.Wakati wa usiku warejeshe kwa mama yao ili awakinge na baridi. Fanya hivi hadi
wafi kie umri wa mwezi mmoja ndipo uwatenge na mama yao.
Pia unaweza kutumia kifaa maalum cha kulelea vifaranga (kitalu) mara baada
ya kuanguliwa. Katika kitalu wanapatiwa joto wanalohitaji. Kifaa hiki kinaweza
kutengenezwakwa karatasi ngumu itumikayo kutengeza dari.(angalia mchoro
unaofuata).
 Au
Katika mazingira ya kijijini unaweza
kutengeneza wigo wa mduara kwa magunia.
Upana wake uwiane na wingi wa vifaranga
ulionao na kina chake kama mita moja. Ukuta
wake uwe na tabaka mbili za magunia hayo
zilizoachana kwa nafasi ya inchi tatu au
nne. Kati kati ya nafasi hiyo jaza maranda ya
mbao au pumba za mpunga. Tayari utakuwa
umepata kitalu cha kulelea vifaranga.
Ndani ya kitalu weka taa ya chemli ya kutoa joto linalohitajika kwa vifaranga.
Fuatilia tabia ya vifaranga wanapokuwa katika kitalu.
Wakiisogelea sana taa ina maana joto halitoshi, ongezea joto kwa kupandisha utambi.
Wakienda mbali sana na taa, joto limezidi punguza. Kitalu kikiwa na joto zuri vifaranga
watatawanyika kote katika kitalu na kuonyesha kuchangamka.
Kulea vifaranga kwa kumtumia kuku
Kulea vifaranga kwa kumtumia kitalu 12
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Mama yao akitengwa na vifaranga arudishwe kwenye kundi lenye jogoo, atapandwa
na kurudia kutaga mapema. Kwa njia hii kundi la kuku litakuwa kubwa kwa muda mfupi.
Kwa kawaida vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na baridi,
kuliwa na wanyama wengine na magonjwa.
Ili kudhibiti magonjwa, vifaranga wapewe chanjo dhidi ya magonjwa yafuatayo:
a. Kideri ( New castle) siku ya 3 baada ya kuanguliwa, rudia baada ya wiki tatu kisha
uchanje kila baada ya miezi mitatu.
b. Kuhara damu au rangi ya ugoro (Coccidiosis) : Wapewe kinga kwa dawa ya
Amprolium kwa siku 3 mfululizo wanapofikisha umri wasiku 7 baada ya kuanguliwa.
c. Gumboro wanashusha mbawa na kujikusanya pamoja kwa baridi, pia wanaharisha
nyeupe.Hutokea kuanzia wiki ya 2 hadi ya 18.Wapewe chanjo siku ya 10 hadi ya 14
baada ya kuanguliwa na rudia baada ya siku 28 na 42. Kwa magonjwa mengine
angalia maelekezo sehemu ya magonjwa ndani ya mwongozo huu.
Vifaranga wapewe chakula kilichoelezwa katika sehemu ya tatu ya kijitabu hiki na
maji safi ya kutosha wakati wote kwa muda wa miezi miwili. Baada ya hapo wanapewa
chakula cha kuku wanaokua.
Kuku wakikaribia kupevuka wakiwa na miezi mitatu hadi minne tenganisha temba
na majogoo ili kudhibiti kuku wenye uhusiano wa damu wasipandane wao kwa wao.
Wakipandana na mayai yao yakianguliwa hawatatoka vifaranga wenye sifa nzuri mfano:
ukuaji wao utakuwa hafifu kuliko wazazi wao, uwezo mdogo kuhimili magonjwa na
wengine wanaweza kuwa na ulemavu. Pia zingatia matemba hao wasipandwe na baba
yao. Vilevile majogoo hao wasimpande mama yao. 13
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Kiini lishe
Wanga
Mafuta
Protini
Vitamini
Madini (calsium
na Fosforas)
Kinapatikana katika chakula gani
Pumba,Chenga za nafaka kama
mahindi, mtama.
Mashudu yanayopatikana baada ya
kukamua mbegu za mafuta kama
alizeti, karanga n.k
Mashudu ya karanga au alizeti.Damu
iliyokaushwa ya wanyama kama
mbuzi, ng’ombe n.k. Mbegu za jamii
ya mikunde kama maharage, kunde,
soya....
Majani mabichi kama mabaki ya
mboga za majani, michicha ya porini,
majani mabichi ya mipapai, majani ya
Lusina n.k.
Unga wa dagaa, unga wa mifupa
iliyochomwa, chokaa
Kazi yake mwilini
Kutia nguvu mwilini
Kutia nguvu na joto
mwilini
Kujenga mwili na
kukarabati mwili
Kulinda mwili. Majani
mabichi pia huwezesha
kuku kutaga mayai yenye
kiina cha njano, rangi
ambayo huwavutia walaji
wengi.
Kujenga mifupa,
kutengeneza maganda
ya mayai
Sehemu ya Nne
Utunzaji wa Kuku
Ulishaji
Kuku kama mifugo mingine uhitaji chakula chenye virutubisho vyote vinavyohitajika
mwilini ili kukua upesi na kuwa na na afya nzuri . Chakula kinachofaa ni mchanganyiko
wa viini lishe mbalimbali vyenye kazi tofauti mwilini. Kila kiini lishe hakina budi kiwe
katika kiwango sahihi kulingana mahitaji ya mwili wa kuku katika umri tofauti.
Kuku anahitaji chakula chenye viini lishe vifuatavyo: 14
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Mfano wa kuandaa vyakula vya makundi tofauti ya kuku
Kwa Vifaranga
Kwa vifaranga vya tangu kutotolewa hadi miezi miwili tengeneza mchanganyiko ufuatao.
Huu ni mfano mmojawapo wa kuandaa kilo 100 za chakula cha vifaranga. Iwapo utahitaji
kuandaa jumla ya kilo 50 za chakula tumia nusu ya vipimo vilivyoainishwa katika jedwali
hili.
Wastani wa mahitaji ya kuku wakubwa 50 kwa siku ni kilo 5. Chakula hiki ukigawe katika
sehemu mbili na kuwapatia nusu asubuhi na nusu ya pili mchana.
Vifaranga hupewa chakula kiasi wanachoweza kumaliza (hawapimiwi).
Vifaa
Dagaa (unga au vichwa vya dagaa)
Chenga za nafaka kama mahindi au mtama n.k
Mashudu
Pumba
Chokaa
Unga wa Mifupa,Madini ( Premix)
Chumvi
Mchanga
Jumla
Kiasi kwa kilo
12 hadi 15
40
20
24
2
2
Robo kilo
1
Kilo 100
Vifaa
Dagaa (unga au vichwa vya dagaa)
Chenga za nafaka kama mahindi au mtama n.k
Mashudu
Pumba
Chokaa
Unga wa Mifupa,Madini ( Premix)
Chumvi
Mchanga
Jumla
Kiasi kwa kilo
7
30
20
39
2
2
Robo kilo
1
Kilo 100
Kwa kuku wanaokua (baada ya miezi miwili ).15
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Kama umeamua kufuga kuku kwa mtindo wa kuwaacha huru wajitafutie chakula (huria)
unaweza kuwapatia vifaranga nyongeza ya protini.Utafanya hivyo kwa kuwachanganyia
vumbi au vichwa vya dagaa kiasi cha kikombe kimoja vilivyotwangwa pamoja na pumba
ya mahindi vikombe vitano.
Maji ya Kunywa
Mfugaji ahakikishe anawapatia kuku maji masafi ya kunywa na ya kutosha kila siku.
Vyombo vya maji ya kunywa budi visafishwe vizuri kila siku. Hii itasaidia sana kudhibiti
magonjwa yanayoweza kutokana na vimelea vya magonjwa vinavyostawi katika maji
yasiyo safi. Kuku wanaweza kuwekewa maji katika aina tofauti ya vyombo kutegemea
na urahisi wa kupatikana mfano sufuria, ndoo za plastik zilizokatwa kuruhusu kuku
kunywa bila kuchafua.
Usafi katika banda
Matandazo yanayowekwa katika sakafu ya banda la kuku hayana budi yageuzwe mara
kwa mara kwa wastani wa kila baada ya miezi miwili au mitatu . Wakati mwingine ni
kabla ya kipindi hiki muda wowote yanapoloana na maji. Matandazo uharakisha
kukauka kwa unyevu katika banda unaotokana na kinyesi cha kuku na pia zaidi na maji
yanayomwagika.
Usafi katika banda utasaidia kudhibiti kwa kiasi kikubwa magonjwa mbalimbali.
Kuokota mayai
Usiyaache mayai ndani ya viota kwa muda mrefu, yaokote mara kwa mara ili kuepuka
kuharibiwa kwa mayai hayo na kuku wenyewe. Kuku wanayo tabia ya kula mayai yao
ikiwa chakula unachowapa kina upungufu wa protini.
Vilevile kiasi cha mwanga unaoingia ndani ya banda kikizidi kuku hula mayai au
kudonoana wenyewe kwa wenyewe.Uonapo dalili za namna hii kwenye kundi lako
punguza kiasi cha mwanga kwa kuziba sehemu za madirisha kwa vipande vya magunia
au vipande vya makasha ya karatasi ngumu.
Kama ilivyoelezwa awali kuku wapewe majani mabichi ya kutosha mara kwa mara ili
wawe wanakula hayo badala ya kudonoana.
Pia fuatilia kuhakikiksha kama chakula kina protini ya kutosha. Kama tatizo la kudonoana
na kula mayai litaendelea omba msaada kwa mtaalam wa mifugo akuelekeze jinsi ya
kuwakata au kuwachoma midomo. 16
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Sehemu ya Tano
Magonjwa ya Kuku
Magonjwa ya kuku yapo mengi. Hata hivyo siyo yote yanatokea mara kwa mara hapa
Tanzania. IIi uweze kudhibiti yale yanayotokea katika kundi lako unahitaji kufahamu
dalili za jumla za magonjwa hayo. Unapoigundua moja au zaidi ya dalili za ugonjwa
au wadudu chukua hatua mara moja. Yapo magonjwa ambayo yanaweza kuangamiza
kundi lote la kuku katika.muda mfupi.
Jihadhari na uwezekano wa kupatwa na hasara zinazoletwa na magonjwa ambayo
unaweza kuyazuia.
Katika sehemu hii utajifunza kwa muhtasari tu dalili za jumla za magonjwa ya kuku na
jinsi ya kuyadhibiti.
Dalili za Jumla za Magonjwa ya Kuku
• Kuku kupoteza hamu ya kula.
• Kuzubaa na kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu (Kutochangamka).
• Kushuka kwa kiwango cha utagaji wa mayai.
• Vifaranga kutokua upesi au kudumaa. - Macho kuwa na rangi nyekundu.
• Kujikunja shingo.
• Kutetemeka, kutoa majimaji puani, mdomoni na machoni.
• Kutoa mharo (kinyesi) wa rangi ya kijani au wenye mchanganyiko na damu au cheupe.
• Kukonda.
• Kukohoa.
Ukiona moja au zaidi ya dalili hizi katika kundi lako chukua hatua za kutibu zilizoelezwa
hapa chini. Kama hali ni ngumu zaidi omba msaada kwa mtaalam wa tiba ya mifugo ili
achunguze mara moja na kukushauri jambo la kufanya.
Muhtasari wa Magonjwa Muhimu ya Kuku na Jinsi ya Kuyadhibiti na Kutibu
Ugonjwa
1. Kideri
(Newcastle)
chanzo
Virusi
Kudhibiti na Kutibu
Vifaranga wachanjwe
katika juma lao la
kwanza. Chanjo la pili
wanapofikisha umri wa
miezi 4 na nusu.
Chanja kuku kila baada ya
miezi mitatu.
Dalili
Kukohoa, kupumua
kwa shida.
Mwili
kukosa nguvu; shingo
kujikunja.
Kuharisha kijani.
Kuku hufa wengi
Kuhara damu.17
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Ugonjwa
2. Kuhara damu
(Coccidiosis)
3. Ndui ya kuku
(Fowl pox)
4. Mafua ya kuku
(Fowl coryza)
5. Kuharisha
nyeupe
chanzo
Bakteria
Virusi
Bakteria
Bakteria
Kudhibiti na Kutibu
• Tunza usafi katika
banda.
• Lisha vifaranga chakula
kilichochanganywa
na dawa ya kinga
coccidiost kama
Amprolium au Salfa.
• Watenge kuku wote
Walioambukizwa na
wapatie dawa kama
Amprolium au salfa au
Esb3.
• Kuchanja kuku wote
wakiwa na umri wa
miezi miwili.
• Watenge kuku wote
walioambukizwa na
wapewe antibiotic kama
OTC plus au salfa.
• Usafi wa banda
• Kuchanja kuku wote
• Kabla hawajaambukizwa
kama ni tatizo sugu
katika eneo
• Watibu wanaougua
kwa kutumia anti biotic
kama sulphamethazine,
streptomycine na
vitamin
• Usafi wa vyombo na
banda kwa ujumla
• Watenge kuku
wagonjwa
• Tumia dawa kama
Furazolidone au
Sulfadimidine
• Hata vitunguu
Dalili
Kuku hujikusanya pamoja.
Hawachangamki.
Hushusha mbawa.
Malengelenge kwenye
kishungi na kope za
macho na sehemu zisizo
na manyoya.
Kuku uvimba uso na
macho
Kamasi hutirirka puani na
mdomoni
Kuhema kwa shida hata
kukoroma.
Kukohoa.
Kuharisha nyeupe na
hamu ya kula kupungua.
Wadudu washambuliao
Kuku18
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Viroboto,Chawa,
Papasi
Wadudu washambuliao Kuku
saumu menya robo
kilo utwange nu
kuchanganya na
maji lita moja. Chuja
uwapatie maji haya kwa
muda wa wiki moja.
Wadudu washambuliao
Kuku
Usafi wa banda na
mazingira
Banda lipitishe hewa ya
kutosha ili liwe kavu
Nyunyizia kuku na banda
zima dawa za kuua wadudu
kama vile Akheri powder,
Malathion, Servin n.k
Kuku hawatulii, hujikuna
mara kwa mara.
Hupungukiwa na damu na
uzito
Wadudu huonekana
mwilini
Njia kuu za ujumla za kudhibiti magonjwa ni:
• Kutunza hali ya usafi ndani ya banda na
kudhiditi kusiwe na unyevu
• Matandazo yakichafuka yabadilishwe.
• Vyombo vya maji visafishwe kila siku
• Jitahidi uepuke kufuga kwa njia ya huria
ili kuku wako wasiambukizwe magonjwa
kirahisi
• Epuka kufuga kuku wako pamoja na bata
na khanga.Hawa ni wabebaji wa vimelea
vya magonjwa ya kuku japo wao hubaki
salama.
• Zingatia ratiba za chanjo kwa magonja
yasiyo na tiba kama kideri na mengineyo
ya virusi
Kutoa chanjo ya kideri kwa njia ya kuweka matone ya dawa katika macho
Kutoa chanjo ya kideri kwa njia ya kuweka
matone ya dawa katika macho 19
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Sehemu ya Sita
Kusimamia Ufugaji Wako
Kutunza kumbukumbu
Ili ufanikiwe katika ufugaji wa kuku, ni muhimu sana kulifahamu vyemi kundi la kuku
wako. Ukilifahamu vema kundi lako utaweza:
Kuchagua kuku bora wa kuzalishia kwa kuangalia ubora wa wazazi wao.
Kufahamu historia ya afya ya kundi, kwa mfano
• Umri ambapo vifaranga vilipata chanjo.
• Ni chanjo ya aina gani.
• Magonjwa ambayo yamewahi kushuambulia kundi, na dawa ulizotumia katika
matibabu.
• ldadi ya kuku wanaokufa.
• Kukadiria kiasi cha chakula ambacho kuku wako watahitaji kwa muda fulani na aina
ya chakula.
• Kujua kila siku kuku wametaga mayai mangapi.
• Kujua utahitaji muda gani kutunza kuku toka vifaranga mpaka wanapofikia kuuzwa.
Ili uweze kufahamu mambo haya yote unahitaji kutunza kumbukumbu
Ufuatao hapa chini ni mfano rahisi wa kutunza kumbukumbu za kuku tangu wangali
vifaranga mpaka wanapofikia uzito wa kuuzwa.
Mfano wa Kumbukumbu za ufugaji wa Kuku
Kumbukumbu ya Vyakula
Tarehe
Jumla
Kiasi cha Chakula
(Kilo)
15
25
Kundi / Umri wa
kuku na idadi yao
Vifaranga
Wanaokua
Maoni (Gharama,
Kimetumika kwa muda gani
nk)20
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Hapa utaweza kujua wastani wa matumizi ya chakula kwa idadi ya kuku na kwa kipindi
husika.
Tarehe ya kuuza……………………….
Idadi iliyouzwa……………………………
Umri wa kuku wakati wa kuwauza................
Mapato kutokana na kuuza……………………
Kumbukumbu ya Kutibu Magonjwa
chanjo au Kudhibiti magonjwa
tarehe
3.7.2009
5.9.2009
tarehe
6.8.2009
5.10.2009
Magonjwa
coccidiosis
mdondo
Ugonjwa/Wadudu
Viroboto
coccidiosis
tiba
teramycin
furazolidone
Dawa
Kunyunyiza doom powder au sevin powder
Amprol katika maji, kinga dhidi ya
Maoni (vifo, gharama nk)
Gharama
Kumbukumbu hii itakusaidia kujua magonjwa yanayosumbua mara kwa mara na kwa
kipindi kipi. Pia na dawa inayosaidia zaidi kwa tatizo husika.
Jinsi ya Kufahamu Faida Unayopata
IIi uweze kufahamu faida unayopata kutokana na ufugaji wa kuku inakupasa kutunza
kumbukumbu za matumizi na mapato ya kila siku.
Kwa mfano:
Upande wa matumizi ingiza
• Gharama ya kununua vifaranga (kama walitotolewa hapo hapo nyumbani inafaa
ukadirie gharama hiyo).
• Gharama ya chakula. 21
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Mapato
Mauzo ya mayai 10
@150/=
Mayai na kuku
waliotumiwa
nyumbani
Mauzo ya kuku 20
@ 4000/=
Mbolea iliyouzwa
…. nk
Kumbukumbu ya Kutibu Magonjwa
tarehe
Jumla
Matumizi tarehe
Kununua vifaranga
30 @ 200/=
Kununua vyakula
kilo 10 @150/=
Dawa ya kukohoa
1500/=
Dawa ya wadudu
1000/=
 ……nk.
Sh.
6,000/=
1,500/=
1,500/=
1000/=
….. nk
Sh.
1,500/=
7,000/=
80,000/
• Kama unatengeneza na kuchanganya wewe mwenyewe kadiria kwa kutumia bei za
viungo ghafi.
• Gharama ya mafuta ya taa (kama uliwakuza vifaranga kwa joto Ia taa).
• Gharama ya kusafisha banda kubadili matandazo.
• Gharama za madawa ya kinga (chanjo) na tiba.
Upande wa mapato ingiza mapato kutokana na:
• Mauzo ya mayai.
• Mauzo ya kuku hai.
• Gharama ya mayai yaliyotumiwa nyumbani.
• Mauzo ya mbolea kutoka katika banda.
Ufuatao ni mfano unaoonyesha jinsi ya kuingiza taarifa hizi katika daftari la kumbukumbu
.
Baada ya kufanya mauzo yote ya kundi jumlisha matumizi yote na jumlisha na mapato
yote katika kipindi kizima cha kufuga.
Ili kufahamu faida uliyopata fanya hesabu hii:
Jumla ya Mapato yote - Jumla ya Matumizi yote = Faida 22
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Sehemu ya Saba
Masoko
Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi
yatakayomsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara
anayoifanya:
Kwanza kabisa ajiulize kama bidhaa anayozalisha ina soko? Na kama soko lipo:
• Lipo wapi na hali ya miundombinu za kulifikia iko vipi ( ili afahamu gharama ya kufika
sokoni kama utaamua kuuzia sokoni).
• Bidhaa inahitajika kwa wingi kiasi gani na wakati gani sokoni
• Soko linahitaji bidhaa yenye sifa zipi ( ubora n.k. ili uzalishe sawa na matakwa ya soko
n.k)
• Kama wanunuzi watakuwa na utayari kununulia unakozalishia, je unao uwezo wa
kutosheleza mahitaji yao (ili uweze kujipanga kukidhi mahitaji kwa kuongeza uzalishaji
au kwa kuungana na wazalishaji wengine).
• Linganisha bei ya bidhaa sokoni na bei ya kuuzia unakozalishia (ili ujue palipo na faida
zaidi kwako baada ya kuondoa gharama za kufuata soko) Ila ukiamua kuuzia sokoni
hakikisha unao uwezo wa kushindana na wauzaji wengine huko sokoni.
Majibu ya maswali haya ndiyo yatakayokupa msingi wa kujipanga kiuzalishaji ili hatimaye
upate faida. Hivyo hata kabla hujaanza kuzalisha fahamu haya yaliyotajwa hapa juu.
Kutafuta na kutumia taarifa za masoko ya sehemu tofauti
Kwa kadri utakavyokuwa unaendelea kuzalisha, mabadiliko mbali mbali yatatokea
kuhusiana na uzalishaji wako na hata kuhusiana na soko la bidhaa unayozalisha kwa
maana ya kuku.
Ili uendane na mabadiliko yanayotokea ni muhimu mzalishaji upate taarifa za hali ya
soko mara kwa mara. Taarifa hizi zitakusaidia kufanya maamuzi yatakayokuwezesha
kuendelea kupata faida.
Taarifa za masoko zinaweza kupatikna kwa wazalishaji kadhaa kuungana na kuunda
umoja wao. Katika umoja huo wawakilishi wachache wanakuwa na jukumu la kutafuta
taarifa za masoko ya kuku sehemu mbali mbali ambako kunaweza kuwapa wazalishaji
tija zaidi.
Walio katika umoja huo watatumia taarifa hizo kufanya maamuzi ya kuuza kwa faida
zaidi kwa pamoja au kwa mmojammoja kutegemeana na hali halisi. Watoa taarifa pia 23
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
watafanya mawasiliano ya kuwajulisha wanunuzi juu ya upatikanaji wa kuku kwenye
maeneo wanakozalishiwa.
Mbinu zaidi ya kupata masoko mazuri
Umoja wa kuzalisha na kuuza
Kwa kawaida kama bidhaa ina soko, wateja hupatikana kwa urahisi pale wanapohakikishiwa
upatikanaji wa bidhaa kwa wingi katika sehemu moja.
Katika hali hii, wanunuzi huwa tayari hata kununua kwa bei ya juu zaidi kwa sababu ya
kupunguza muda na gharama ya kutafuta bidhaa ya kutosha kupeleka sokoni.
Kwa upande wa kuku jambo hili linawezekana kama mfugaji atafuga kuku wengi wa umri
usiopishana sana kwa wakati mmoja. Watakapofikia kimo kinachofaa kuuza utawauza
wengi kwa wakati mmoja na kwa faida zaidi.
Mahali ambapo mfugaji mmoja mmoja hawezi kukidhi wingi wa hitaji la wanunuzi,
wafugaji kadhaa wanaweza kuunda umoja wao wa kuzalisha (kila mmoja kwake ) na
kuuza kwa kipindi kimoja na kupata faida zilizotajwa hapa juu.
Faida nyingine ya kuuza katika umoja ni kuongezeka kwa uwezo wenu wa kupanga na
kusimamia bei mnayotaka kuuzia. Sauti na uamuzi wenu wa pamoja utawapa nguvu ya
kusimamia bei yenu mnayoipanga dhidi ya bei za chini wanazotaka wanunuzi. Uwezo
wako wa kusimamia bei unyoitaka ni mdogo ukiuza peke yako. 24
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Sehemu ya Nane
Chama cha Akiba na Kukopa
Chama cha akiba na mikopo ni kikundi cha watu waliojiunga kwa hari yao kufanya
ushirika wa kuweka akiba zao kwa pamoja na kutoa mikopo kwa urahisi kutokana na
akiba zao.
Kwa wafugaji wa kuku kubiashara wanashauriwa kuwa na chombo cha namna hii
kitakachokuwa na utaratibu wa wanachama kuweka na pia wanachama hawa kuwa na
fursa ya kukopa kwa lengo kubwa la kuendeleza ufugaji wao kuku kibiashara.Ufugaji
wa kibiashara ungehitaji kuongeza mtaji mara kwa mara kulingana na mahitaji ya soko
husika. Mfumo wa kuweka na kukopa utakuwa chanzo kizuri na cha kuaminika kukidhi
haja ya mtaji endelevu kwa wafugaji wa kuku.
Michango kwa ajili ya akiba inaweza kutokana na makato ya mapato yanayotokana na
mauzo ya bidhaa za kuku ( vifaranga,mayai, kuku n.k. ). Au kiwango maalum kwa wakati
maalum kinaweza kuwekwa na wanachama ili kitolewe kwa utaratibi wanaokubalianana.
Wanachama wanaweza kukopa kutoka kwenye chama chao kwa ajili ya ununuzi wa
mahitaji,mbalimbali ya kuku kama:
• Madawa
• Vyakula
• Ukarabati au ujenzi wa mabanda ya kuku n.k
Faida za chama kama hiki ni:
• Wanachama watapata sehemu ya kuhifadhi pesa yao kwa usalama kwa ajili ya
matumizi ya baadaye.
• Masharti ya kukopa ni nafuu kuliko vyombo vingine vya kifedha.
• Wanachama hujifunza misingi ya kushirikiana, mahusiano na kusaidiana.
• Wanachama hupata maarifa ya ziada kuhusu maswala ya kifedha.
Chama cha namna hii, lazima kiwe na kanuni za kukiongoza ambazo hutungwa na
wanachama wenyewe.
Kanuni hizi zilenge kulinda malengo ya chama na kila mwanachama anawajibika
kuzizingatia.25
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili
Mambo makuu ya kuzingatia katika katiba ni:
• Malengo ya chama
• Haki, wajibu na malengo ya wanachama
• Viwango vya viingilio
• Hisa na michango
• Uongozi na majukumu
• Vikao na mikutano
• Utunzaji wa kumbukumbu
• Mikopo na riba
• Taratibu za kutoa mikopo
• Migawanyo ya faida
Mambo ya msingi ya kusimamia na kuendesha chama cha Akiba na Kukopa ni pamoja
na:
o Uhiari wa wanachama
o Uongozi uwe wa kidemokrasia
o Kusiwe na urasimu
o Chama lazima kiwe na vitabu vitakavyotumika kuweka kumbukumbu ya hifadhi za
fedha za wanachama
o Uwekaji wa akiba uwe wa mara kwa mara
o Mkopo ulipwe kwa muda uliopangwa
o Fedha za chama ziwekwe benki au kwenye masanduku maalum ya kutunzia kwa
utaratibu uliopendekezwa Mahesabu ya chama yafanyiwe ukaguzi mara kwa mara.
Kikundi kama hiki kinaunganisha nguvu pamoja na kupunguza tatizo la kupata huduma
ya kifedha hasa katika maeneo ya vijijini.Hata hivyo jambo la msingi la kufanikisha
malengo ya vyombo hivi ni kuzingatia kanuni zilizowekwa na wahusika. Vilevile utaalam
wa kutosha wa kuendesha na kusimamia chombo vya namna hii ni muhimu uwepo. 26
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili27
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili28
Ufugaji Bora Wa Kuku Wa Asili

Share this article :

Chapisha Maoni

 
Copyright © 2013. KCC KIBAHA - All Rights Reserved
Template Created by KIJANA WA LEO Published by TITUS KAPOMA
Proudly powered by Blogger