Jumanne, 11 Juni 20130 comments

1
Biasha
 
 
ra ya kuku wa asili
Mwongozo kwa mfugaji
Biashara ya kuku
wa asili
Mwongozo wa uuzaji wa kuku na
Mazao yake kwa Mfugaji

 
 
 
 

 
 
 
 
 
 
2
Biashara ya kuku wa asili
rl
DC na
u
boreshaji wa Maisha Vijijini
Shirika la Rural Livelihood Development Company (RLDC ni moja ya mafanikio
ya ushirikaiano kati ya Tanzania na Uswisi kwenye mchakato wa kupambana na
umaskini na kuboresha maisha ya jamii za vijijini. Hii ni taasisi isiyo ya kibiashara
ili yoanzishwa mwaka 2005 na mashirika ya Intercooperation na Swisscontact,
lengo kuu likiwa kutekeleza Programu ya kuendeleza maisha ya jamii za vijijini
(RLDP). Programu hii inasha bihiana na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupambana
na Umaskini (MKUKUTA). Dhamira kuu ya RLDC ni Kuendeleza/kuboresha mifu
mo ya masoko ili kuwawezesha wazalishaji wa vijijini kutumia
fursa zilipo kuboresha maisha yao.
Kwa sasa, RLDC inatelekeleza awamu ya pili ya mpango wake (2008-2011)
na inaweka msukumo zaidi kwenye uendelezaji wa mifumo ya masoko. RLDC
inafanya kazi katika mikoa sita ya Kanda ya kati-Dodoma, Singida, Morogoro,
Shinyanga, Tabora, na Manyara. Jamii nyingi maskini zinaishi katika ukanda huu
wenye sehemu kubwa yenye hali ya mvua chache na nusu jangwa inayostawisha
shughuli chache za kiuchumi.
Hata hivyo kuna fursa nyingi sana zinazoweza kutoa ajira na kuboresha ya
jamii zake. RLDC inafadhiliwa na Serikali ya Uswisi kupitia shirika la Uswisi la
maendeleo (SDC).
Kwa sasa RLDC inawezesha sekta za pamba, alizeti, maziwa, ufugaji wa kuku wa
kienyeji, mpunga na habari kupitia vipindi vya redio kwa ajili ya wazalishaji wa
vijijini.
rl
DC inaboresha mifumo ya masoko ili kuwezesha wazalishaji wa
vijijini kuinua maisha yao”
Biashara ya kuku
wa asili
Mwongozo wa uuzaji wa kuku na
M
azao
yake kwa
M
fugaji
4
Biashara ya kuku wa asili
YALIYOMO
Utangulizi
1
Mbinu tofauti za kupata masoko mazuri
2
Kufanya makubaliano
2
Kuandaa mazingira mazuri ya soko kijijini
2
Nini kifanyike ili soko la ndani/ kijijini liwe endelevu?
2
Kuandaa na kusafirisha mayai na kuku
2
Mbinu bora za kusafirisha kuku
2
1
Biashara ya kuku wa asili
Utangulizi
Kuendelea kwa mradi wa ufugagji kuku na kukua kwa kipato cha jamii zinazojihusisha na
ufugaji wa kuku vijijini kunategemea ubora wa kuku na mazao yanayozalishwa pamoja
na soko zuri. Mahitaji ya kuku na mayai ya asili yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku
kutokana na ladha nzuri ya nyama na mayai hayo pamoja na uhalisi wake. Hii ndiyo
sababu (au fursa) ya msingi inayoshawishi kuendelea kuzalisha mazao haya.
Pamoja na kuwepo kwa fursa hizi bado zipo changamoto nyingi katikati eneo la soko
la mazao ya kuku wa asili. Changamoto hizi zinafanya mfugaji asinufaike kiasi cha
kuridhisha kutokana na ufugaji wake.
Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na:
Wafugaji kutokuwa na maamuzi katika kupanga bei ya mazao yao.
Wafugaji kukosa taarifa za bei za kuku wa asili na mayai kwenye masoko mbalimbali.
Kuna idadi kubwa ya wanufaikaji kabla bidhaa haijamfikia mlaji wa mwisho
(mlolongo mrefu wa soko).
Gharama kubwa za usafiri na usafirishaji kwenda sokoni kutokana na hali mbaya
ya miundo mbinu.
Ili mfugaji aweze kupata faida inabidi awe na mbinu za kukabiliana na changamoto hizi
za soko. Katika mwongozo huu yanaelezwa mambo ya kusaidia uuzaji kwa faida baada
ya kuzalisha kuku na mayai.
Mbinu tofauti za kupata masoko mazuri
Kuwa na umoja/mtandao wa wazalishaji na wauzaji wa kuku wa asili
Umoja huu utasaidia kuwawezesha wafugaji kuwa na sauti ya pamoja kupanga na
kusimamia bei ya mazao yao. Upangaji wa bei utazingatia gharama zote za uzalishaji ili
mfugaji apate faida ya kuridhisha. Hii itawezekana kama kuku/mayai yanauzwa katika
sehemu mmoja watakayokubaliana wafugaji.
Share this article :

Chapisha Maoni

 
Copyright © 2013. KCC KIBAHA - All Rights Reserved
Template Created by KIJANA WA LEO Published by TITUS KAPOMA
Proudly powered by Blogger